Kikosi
cha mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans ‘Yanga’ kinaendelea kujifua
kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya SC Villa ‘vijogoo’
pambano litakalopigwa kesho (Jumamosi) kwenye uwanja wa Taifa.
Katibu
mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema watawarejesha wakali wao ambao wapo
kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stsrs’ ili waungane na wachezaji wengine
kwa ajili ya kuikabili SC Villa kwenye mchezo utakaopigwa kesho kwenye uwnja wa
Taifa.
“Kikosi
kinaendelea vizuri ila wachezaji wetu wengi wameondoka wameenda kujiunga na
kikosi cha timu ya Taifa lakini tumepeleka barua TFF kuwaomba wawaruhusu leo
jioni ili waweze kukutana na wenzao kwenye ‘camp’ kwa ajili ya mchezo wa
Jumamosi na SC Villa”, amesema Tiboroha.
Kuhusu
suala la kumsajili mchezaji anaefanya majaribio kwenye kikosi cha Yanga ambae
ni raia wa Sierra Leone Lansana Kamara, Tiboroha amesema, mchezaji huyo ni
mzuri lakini majukumu yote ya kumsajili au kutomsajili yapo chini ya waalimu.
“Kama
jinsi ilivyo kwa hao wengine unasikia anaongelewa kwamba wanakuja, hawaji,
lakini tunatakiwa tuwe wangaalifu kidogo maana kumbuka tuliomba nafasi kumi
lakini tumepewa sabakwa maana hiyo katika nafasi zile kumi tulizoomba tulikuwa
na uwezo wa kuongeza wachezaji watano. Lakini sasahivi hatuna uwezo huo, tuna
uwezo wa kuongeza wachezaji wawili tu”, ameongeza.
“Tunampa
mwalimu muda ajiridhishe, awaangalie wachezaji alionao aendelee kupata ‘report’
za huku na kule ili aweze kuangalia ‘statistics’ namna gani zinavyokwenda ili
kujua mwishoni tunapoamua tuchukue nani kati ya hao ambao tunataka kuongeza ili
chaguo letu liwe zuri”, amefafanua.
“Nafikiri
uamuzi kuhusu Kamara utatolewa na waalimu, mimi binafsi nimemuona Kamara
mazoezini ni mchezaji mzuri sasa walimu kama wataalamu wetu watakuwa na vigezo
vyao vingine ambavyo wataviangalia ili mwisho wa siku katika hizo nafasi mbili
tunazozitaka awemo, vigezo wanavyovitaka walimu wetu akiwanavyo atakuwemo
katika hizo nafasi mbili”, alimaliza.
0 comments:
Post a Comment