Klabu ya Yanga imethibitisha kuvunja mkataba na
mshambuliaji wake, Said Bahanuzi kutokana na kushuka kiwango kwa miaka mitatu
mfululizo.
Katibu mkuu wa Yanga, Dkt. Jonas Tiboroha amesema
kwamba , Yanga haijaridhishwa na maendeleo ya Bahanuzi aliyekuwa anacheza kwa
mkopo msimu uliopita katika klabu ya Polisi Morogoro, hivyo anatolewa kama
ilivyotokea kwa Jeryson Tegete na Omega Seme.
“Bahanuzi ni moja ya wachezaji tuliovunja nao mikataba
kwasababu klabu haijaridhishwa na maendeleo
yake kama ilivyo kwa wachezaji wenzake akina Omega, Thabit, Jerry Tegete”. Amesema Tiboroha
na kuongeza: “Mikataba ya Yanga inaangalia kiwango cha mchezaji, kama mchezaji hana
kiwango kwa miaka mitatu anaachwa, tunavyo vipengele vinavyoeleza wazi”.
Amesema Toboroha.
0 comments:
Post a Comment