Na Baraka Mbolembole, Dar es
Salaam
KIUNGO-mshambulizi, Deus
Kaseke, mlinzi wa kushoto, Hajji Mwinyi, golikipa, Benedictor Tinocco na
mshambulizi, Malimu Busungu tayari wamesainiwa na Yanga SC kuelekea msimu wa 53
wa ligi kuu na michuanno ya klabu bingwa Afrika mapema mwaka ujao.
Nyota hao wanne kutoka klabu ya Mbeya City FC,
KMKM ya Zanzibar, Kagera Sugar na JKT Mgambo ni mapendekezo ya mwalimu wa timu
hiyo, Hans Van der Pluijm na kwa mara ya kwanza tunaweza kuona Yanga wakifanya
usajili ambao naweza kuuita ' Usajili wa Kitaalamu'.
Tinocco ambaye aliidakia Kagera
msimu uliomalizika Mei mwaka huu ni kipa wa timu ya pili ya Taifa ' Taifa Stars
Maboresho' atachukua nafasi ya mlinda mlango mzoefu, Juma Kaseja ambaye
alijitoa katika timu hiyo miezi 6 iliyopita kwa sababu ya kushindwa kuwa kipa
chaguo la kwanza mbele ya Deogratius Munishi ' Dida' na Ally Mustapha '
Barthez'.
Kwa muda mrefu wapenzi wa timu
hiyo wamekuwa na mashaka na upande wao wa ulinzi ' beki namba 3'. Kimsingi kwa
misimu minne sasa tangu kuondoka kwa Amir Maftah katikati ya mwaka 2011, nafasi
ya mlinzi wa kushoto ' ime-hodhiwa' na Oscar Joshua.
Wakati fulani walitokea Stefano
Mwasyika na David Luhende. Wawili hao ( Mwasyika na Luhende) walikuwa na
mtazamo wa kushambulia zaidi kuliko kuzuia katika uchezaji wao ndiyo maana
walimu, Kostadin Papic, Sam Timbe, Tom Saintfiet, Ernie Brandts na Hans
walipendelea kuwatoa pia katika winga ya kushoto.
Oscar ameifanya Yanga kuwa
ngumu kupitika katika upande wa kushoto, licha ya kutopendelea kupanda na timu
kwenda mbele, Oscar hutumia nguvu zake kushambulia kwa mipira mirefu inayofika
kwa walengwa.
Lakini Yanga haikupaswa
kuendelea kumuacha mcheza wa pekee katika nafasi hiyo ndiyo maana mwalimu Hans
wakati fulani alinukuliwa akisema kuwa angependa kuona timu yake ikimsaini kwa
mara nyingine, Luhende ambaye aliachwa katika usajili wa mwaka uliopita baada
ya Mholanzi huyo, Hans kupata kazi Uarabuni.
Mwinyi ni nyongeza katika beki 3
ya Yanga na mchezaji ambaye ataleta changamoto na tofauti kwa Oscar.
Ni mlinzi wa timu ya Taifa ya
Zanzibar na ile ya Tanzania. Wengi tunauchukulia usajili wa Kaseke kama '
mbadala' wa kiungo mshambulizi, Mrisho Ngassa ambaye amejiunga na klabu ya Free
State Stars ya Afrika Kusini, lakini ikumbukwe kuwa Yanga itawapoteza wachezaji
kama Nizar Khalfan ambaye amejiunga na Mwadui FC ya Kahama, Shinyanga, Hassan
Dilunga ameshindwa kumshawishi, Hans licha ya kupewa nafasi ya kucheza mara kwa
mara hivyo naye ataondolewa.
Kaseke ni kiungo ambaye ana
uwezo wa kucheza upande wa kushoto, kulia na hata kiungo wa mashambulizi '
namba 10'.
Yanga ilimuhitaji mchezaji kama
Kaseke ambaye atakuwa na uwezo wa ' kuinyanyua' timu hata ikiwa ' dhohofu' na
kuifungia magoli magoli. Akiwa na miaka 21 sasa, mchezaji huyo amejijenga kimchezo
katika misimu miwili katika kikosi cha City.
Tayari amecheza jumla ya
michezo 51 ya ligi kuu Bara na kufunga jumla ya mabao 8. Ataweza kufanya kazi
ya Ngassa?. Kukimbia kwa kasi katika nafasi, kucheza kwa kuhaha eneo lote la
mashambulizi akijaribu kufunga na kutengeneza nafasi za magoli. Tusubiri na
tuone ila hadi amesajiliwa Yanga tunapaswa kuipongeza timu hiyo kwa usajili
mbadala.
Yanga inahitaji wachezaji
wawili au watatu zaidi wa nafasi ya kiungo. Haruna Niyonzima ni mchezesha timu
mzuri, Salum Telela na Said Juma Makapu ni ‘ injini’ katikati ya uwanja. Hivyo
hakuna wasiwasi sana na kuondoka kwa viungo kama Nizar na Dilunga.
Katika michuano ambayo
inahitaji mbinu tofauti tofauti ili kupata matokeo, Yanga watalazimika pia
kuutengeneza mfumo wa 4-4-2 ili uwasaidie katika Ligi ya Mabingwa na ligi kuu
ijayo. Licha ya kumsaini mshambulizi, Busungu ambaye alifunga mabao kumi akiwa
na Mgambo msimu uliomalizika, Yanga ina washambuaji kama Amis Tambwe, Kpah
Sherman, na wakati mwingine huchezeshwa Saimon Msuva. Ndio walifunga magoli
mengi katika msimu uliopita kutokana na mfumo ‘ ulio wakubali’ wa 4-3-3, lakini
timu hiyo ilishindwa katika michezo mingi dhidi ya timu kubwa kwa kuwa
walibanwa katika njia na hawakuwa na mbinu mbadala.
Katika gemu mbili na Simba SC
walishindwa kufunga na walifunga goli moja tu katika michezo mitatu ya ugenini
katika michuano ya komnbe la Shirikisho Afrika. Kwa nini imekuwa hivyo?.
Jibu ni kwamba wachezaji wa
safu ya mashambulizi katika timu hiyo hawawezi kucheza katika mtindo wa ‘
washambuaji wawili’ kwa sababu wote hawana ujuzi wa kucheza kama mshambulizi wa
pili-Namba 10.
Bahati mbaya kwa Tanzania
hakuna mchezaji ‘ spesho’ ambaye anaweza kubeba majukumu hayo kwa sasa hivyo
watalazimika kusaka ‘ namba kumi bora’ nje ya nchi ilitayewabeba katika michezo
mikubwa.
Jerson Tegete amesaini Mwadui
FC, Hussein Javu na Said Bahanzi muda wao umemalizika hivyo hawatakuwepo msimu
ujao. Usajili wa Busungu umeletwa kuchukua moja ya nafasi hizo ila hautoshi.
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment