Uongozi wa Yanga
imetangaza kuwa, kamwe haitamsajili profesheno yeyote aliyewahi au anaiyechezea
timu za Ligi Kuu Bara na kwamba ni upuuzi mkubwa kuhusishwa na suala la
kumrejesha Emmanuel Okwi kutoka Simba.
Hiyo ni siku chache tangu ivumishwe kuwa Okwi amesajiliwa Yanga kwa ajili
ya msimu ujao wa ligi kuu.
Ukiachana na
Okwi, baadhi ya wachezaji wa kimataifa wanaotajwa kwenye usajili wa timu hiyo
ni Waivory Coast, Pascal Wawa na Kipre Tchetche.
Katibu Mkuu wa
Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amekaririwa na Salehjembe akisema kuwa ili kuepukana na matatizo, wameona
wachukue maamuzi hayo ya kutosajili wachezaji wa kimataifa wanaozichezea au
waliowahi kuzichezea klabu za hapa nchini.
Tiboroha alisema
wanaamini wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kuichezea Yanga ambao
wamepanga kuwaleta kutoka Nigeria, Ghana, Zimbabwe na Sierra Leone ambao wakati
wowote watatua nchini.
“Kamwe
hautakuja kusikia Yanga imemsajili mchezaji wa kimataifa aliyewahi au
anayeichezea klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu nchini hapa.
“Kama wachezaji
wapo wengi tu kutoka kwenye mataifa mbalimbali, ndiyo maana tumepanga kuwaleta
Waghana, Mzimbabwe, Mnigeria na Msierra Leone ambao watakuja kwa ajili ya
kuichezea Yanga.
“Hiyo ni moja ya
mikakati tuliyoipanga Yanga katika usajili wetu wa msimu huu na miaka ijayo,
labda uongozi mpya uingie, lakini siyo huu wetu,” alisema Tiboroha.
0 comments:
Post a Comment