MABINGWA wa kandanda Tanzania bara, Young Africans kesho
wanatarajia kuanza maandalizi ya ligi kuu msimu ujao pamoja na kombe la Kagame
linalotarajia kuanza kutimua vumbi jijini Dar es salaam Julai 11 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amesema mazoezi
hayo yatakuwa yanafanyika uwanja wa Karume, Ilala, Dar es salaam chini ya kocha
mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm aliyetua Dar usiku wa kuamkia leo akitokea
kwake nchini Ghana.
“Kazi imeanza, kesho asubuhi mazoezi ya kwanza yanaanza
Karume, tunaanza pole pole kwasababu wachezaji wetu wengi wapo timu za taifa
zote mbili”. Amesema Dr. Tiboroha na kuongeza: “Wachezaji wengine wa kimataifa
kama Tambwe (Amiss), Niyonzima (Haruna) wapo kwenye timu zao za taifa, lakini
wachezaji wengine kama Kpah Sherman watawasili kesho, ila wengi watawasili
tarehe 16”.
0 comments:
Post a Comment