Tuesday, June 16, 2015

Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaeleza memba wake wa benchi la ufundi kwa msimu huu hakutakuwa na mzaha hata kidogo.

Pluijm raia wa Uholanzi amewataka kufanya kazi kwa juhudi kwa kiwango cha juu ili wahakikishe wanafanya vizuri nyumbani Bara lakini nguvu nyingi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


“Kweli kocha kasisitiza sana kwamba msimu ujao ni kazikazi. Hakutakuwa na nafasi ya utani hata kidogo.


“Ameanza na watu wa benchi la ufundi na baadaye atashuka hadi kwa wachezaji. Kweli anataka tufanya kazi vizuri na kufanya vizuri hapa nyumbani.


“Lakini amesisitiza sana kuhusiana na Ligi ya Mabingwa Afrika na kasema hicho ndiyo kipimo sahihi,” kilieleza chanzo cha uhakika.



Msimu uliopita, Yanga ilionyesha kiwango cha juu kabisa na kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa na mechi mkononi.
16 Jun 2015

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video