Na Ramadhani Ngoda.
Kiungo wa FC Barcelona anayetazamiwa kuiacha klabu
hiyo, Xavi Hernadez amekanusha vikali uwezekano wa yeye kujiunga na mabingwa wa
Ufaransa PSG baada ya kumaliza muda wake katika miamba hiyo ya Hispania.
Xavi ambaye anatazamiwa kucheza mchezo wa mwisho
akiwa na Barcelona katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya
Juventus katika uwanja uwanja wa Berlin, amewekanusha taarifa zilizotolewa na
vyombo vya habari nchini Ufaransa kuwa anaweza kujiunga na PSG kwa mkopo kabla
kutimkia katika klabu ya Al Sadd ya Qatar aliyoingia nayo mkataba wa miaka
miwili.
“Sitaichezea PSG,” Xavi aliliambiwa gazeti la Al-watan
la nchini Qatar.
Habari za kiungo huyo kujiunga na PSG zilitiwa
nguvu na ukweli kuwa mmiliki wa klabu hiyo ni kaka wa mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi.
Xavi aliisaidia Barcelona kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey waliposhinda
3-1 dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wa fainali jumamosi iliyopita.
Kama Barcelona watafanikiwa kuifunga Juventus katika mchezo
wa fainali ya ligi ya mabingwa siku ya Jumamosi, itakuwa ni taji la 4 kwa veteran
huyo akiwa na Barcelona kwani mpaka sasa tayari amekwishinda mataji matatu ya
ligi hiyo.
Xavi amefikia uamuzi wa kuachana na Bacelona baada ya
kuitumikia kwa takriban maisha yake yote ya soka na kufanikiwa kushinda mataji
nane ya La Liga na matatu ya Copa Del Rey.
0 comments:
Post a Comment