Lowassa ni miongoni mwa makada wa CCM waliotangaza nia na alisema ataboresha michezo ingawa hakuanisha sera madhubuti
WAKATI vuguvugu la watu kutangaza nia ya kuomba kugombea
nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) likiendelea, Rais wa kampuni ya ngumi za kulipwa nchini, TPBO, Yassin
Abdallah ‘Ustadh’ amewashukia makada wa chama tawala kwa kushindwa kueleza sera
madhubuti juu ya kuendele za michezo nchini.
Yassin amesema kwamba amewasikiliza Watangaza nia wote na
kuona wanagusiagusia tu michezo hususani soka, lakini wamesahau michezo mingine
isiyokuwa na udhamini mfano Ngumi.
“Watangaza nia wote ni waelezaji wazuri sana kwa maana ya
medani ya kisiasa, lakini bado suala la michezo wanagusiagusia tu, hakuna
ambaye amezungumza kiundani ni vitu gani atawafanyia Watanzania kwenye michezo.
Ukiangalia wote wanazungumzia soka, kwani Tanzania ni nchi ya mpira wa miguu
tu? Kuna michezo mingi ambayo haina udhamini kama ngumi, riadha, tenisi, mpira
wa kikapu nk”. Amesema Yassin .
“Sijaona mtu
akizungumza kiundani kuhusu michezo, wengine wanasema Wataifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda, wanasahau kuwa michezo ni kiwanda cha kutengeneza ajira, wapo
watu wengi wanalipwa mabilioni kwenye michezo. Maneno yao mimi naona ni siasa
tu, ukiangalia viwanja vingi kwasasa vimejaa Diwani Cup, Mbunge Cup, lengo ni
kuwashawishi wapiga kura tu, baada ya uchaguzi hakuna jipya”.
0 comments:
Post a Comment