MOJA ya safu kali zaidi ya ushambuliaji kuwahi kutokea
duniani ni ya FC Barcelona inayojumuisha ‘mastraika’ watatu, Lionel Messi, Luis
Suarez na Neymar Jr.
Safu hii inayowasha moto wa hatari imepewa kifupicho cha MSN
yaani Messi, Suarez, Neymar.
Mbali na uwezo binafsi wa kila mchezaji alioonesha msimu huu
katika kikosi chao na kuisaidia Barca
kubeba La Liga, Copa del Rey na Uefa Champions League, Messi, Suarez na Neymar wamekuwa
marafiki wazuri ndani na nje ya uwanja.
Kutokana na muunganiko wao wa kiuchezaji, wanasoka hao
wamekuwa gumzo kubwa katika ulimwengu wa
soka na kusababisha wachambuzi wa michezo kwenda mbali zaidi wakijaribu
kuelezea karama zao kubwa.
Mtando wakimichezo “talksport” sasa umeamua kuhusianisha miji waliyozaliwa
wachezaji hao kwa kuonesha Geographia ya makazi ya wanasoka hao watatu.
Baada ya kuchoro ramani na kuweka alama kwenye miji yao, wakachora
mstari mmoja ulionyoka ‘Straight line’ kutoka
mji anaotoka Messi(Argentina), Suareza (Urguay) na Neymar(Brazil).
Baada ya kuona mstari huo umenyooka, wamedai kuwa
inawezekana ndio sababu ya washambuliaji hao kuwa na muunganiko wa ajabu katika
safu ya ushambuliaji.
Angalia ramani yenyewe hapa chini;
0 comments:
Post a Comment