KIKOSI cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi leo kujiandaa
kwa ajili ya kuivaa Misri Juni 14.
Stars imefanya mazoezi leo lakini leo saa
11 jioni ina safari ya kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya kambi.
Stars itaweka kambi nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo huo dhidi ya Misri kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Kocha Mart Nooij ndiye aliongoza kikosi hicho katika mazoezi
ya leo licha ya kuwa waandishi walizuiwa kuingia.
Salehjembe ameripoti
kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakizuiwa na uongozi wa Gymkhana kwa madai si
wanachama wa klabu hiyo.
Hata hivyo wamekuwa wakiomba kupewa ruhusa angalau ya
kufanya kazi yao kwa kushuhudia mazoezi ya Stars tu kwa takribani saa mbili,
halafu waondoke, lakini imekataliwa kabisa.
Haijajulikana kwa nini hali hiyo inatokea wakati Gymkhana
wamekuwa wakiawaalika waandishi katika michuano mbalimbali inayofanyika klabuni
hapo.
Askari waliendelea kusisitiza kuwa waandishi hawaruhusiwi
kuingia na TFF wanalijua suala hilo.
0 comments:
Post a Comment