Uwanja wa St Georges Park umekuwa 'busy' sana wiki hii ambapo timu ya taifa ya wakubwa ya England 'Simba watatu', timu ya vijana chini ya miaka 21 na timu ya taifa ya wakubwa ya soka ya Wanawake zimekuwa zikifanya mazoezi Birmingham HQ.
Simba Watatu wanajiandaa na mechi ya kesho ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016) dhidi ya Slovenia na tayari wameshashinda mechi zote tano za mwanzo kwenye kundi lao na wakishinda kesho watakuwa wamefuzu mapema kabisa.
Katika mazoezi ya wiki nzima, wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi ya kupiga mashuti golini na hapa chini na magoli matano ya wiki kutoka katika mazoezi hayo, huku goli la Wayne Rooney likishika namba 3.
0 comments:
Post a Comment