Mshambuliaji
wa zamani wa Manchester United, Radamel Falcao hajaweka wazi kama anatua
Chelsea, lakini kauli yake imethibitisha kwamba anaweza kujiunga na mabingwa
hao wa England majira ya kiangazi mwaka huu.
Baada ya
Colombia kushinda 1-0 dhidi ya Brazil katika mechi ya Copa America , Falcao
ameulizwa swali kuhusu tetezi zinazoendelea kuhusu yeye kuhamia Chelsea ambapo
amejibu kwamba, inaweza kuwa kweli,
lakini itajulikana siku chache zijazo.
Chelsea
chini ya Jose Mourinho siku chache zijazo inatarajia kutangaza kumsajili Falcao
kwa mkataba wa mkopo wa mwaka moja kutoka Monaco ya Ufaransa, kikiwemo
kipengele cha kumnunua moja kwa moja siku za usoni.
Hata hivyo
baada ya nyota huyo kushindwa kuonesha cheche Manchester United, mashabiki wa
Chelsea wanaamini Falcao atakuwa kama Fernando Torres aliyeshindwa kutamba
Stamfird Bridge.
0 comments:
Post a Comment