Video hii imetoka katika sare ya 2-2 waliyopata Argentina dhidi ya Paraguay kwenye michuano ya Copa America ambapo Lionel Messi na Angeli Di Maria wameonekana wakimcheka kocha mkuu wa timu ya taifa, Tata Martino wakati wanaingia uwanjani kipindi cha pili.
Wakiwa wametoka uwanjani wakiongoza 2-0, Messi alimuuliza Angel Di Maria kwamba ni upuuzi gani kocha alikuwa anaongea wakati wa mapumziko?
Di Maria alimwambia Messi kwamba Tata Martino alisema sio rahisi kushinda mechi hiyo....wote wakacheka.
Leo Messi: "Alikuwa anasema nini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo? ni upuuzi tu".
Angel Di Maria: Alisema sio rahisi kupata matokeo". (wote wakacheka).
Kitendo hicho kimewauzi Waargentina wengi pamoja na kocha Martino na imeripotiwa kuwa wamekalia kiti cha moto.
Tazama Video hiyo hapo chini:
0 comments:
Post a Comment
Links to this post
Create a Link