Stori mbaya imeibuka asubuhi ya leo ikimuhusu kiungo wa Juventus na Chile Arturo Vidal ambaye amepata ajali na gari yake ya thamani aina ya Ferrari kutokana na kuendesha akiwa amelewa pombe.
Arturo ambaye ameifungia Chile magoli matatu katika mechi mbili za Copa America ameripotiwa kupiga pombe aina ya whilst maeneo ya Santiago.
Vidal amenusurika katika ajali hiyo na amekamatwa na Polisi ambao wamempeleka mahakamani leo asubuhi kujibu mashitaka ya kuendesha gari akiwa amelewa kinyume na sheria.
Msemaji wa Jeshi la Polisi la Chile, Colonel Ricardo Gonzalez amethibitisha: " Dereva wa gari lenye rangi nyekundu alikuwa anaendesha akiwa amelewa pombe".
Chile itakabiliana na Bolivia Ijumaa ya wiki hii na taarifa zinasema kiungo huyo mwenye kipaji kikubwa anaweza kucheza mechi hiyo ya mwisho.
Tazama video ya habari hii hapa chini;
0 comments:
Post a Comment