Cristiano Ronaldo hapendi kuzungumzia maisha yake binafsi , lakini ameamua kufunguka ya moyoni akiwa kwenye mapumziko.
Ronaldo amezungumzia kuhusu vyombo vya habari kumuandika kuwa ana wapenzi wengi, lakini hajasahau kutoa shukrani kwa mashabiki zake.
Huu ni ujumbe alioutoa na chini kuna video yenyewe.
"Hi fans…hii meseji ni kwa ajili yenu. Asante sana kwa kunipa support mwaka huu ambao ulikua mgumu lakini siku zote mlikuwepo kwa ajili yangu. Nipo hapa nimepumzika na mwanangu yupo kwenye pool,lakini inakuja tu kichwani mwangu nifanye hii video, lakini sijui kwanini na usiniulize kwanini. Unajua siongeagi kuhusu maisha yangu binafsi kwenye vyombo vya habari".
"Lakini nataka niseme, wiki chache zilizopita vyombo vya habari vilikuwa vinasema mambo mabaya kuhusu mimi kwamba kila siku nina wapenzi wapya. Naomba mniache nifanye kazi yangu vizuri kama ninavyofanyaga. Msijaribu kuharibu jina langu kwasababu haitakuja kutokea. So ujumbe huu ni kwa ajili yenu watu wangu, tupo pamoja siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi mwaka baada ya mwaka, Asanteni.
0 comments:
Post a Comment