kwa mujibu wa data zilizochapishwa na taasisi ya CIES Football Observatory, mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kwasasa ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwenye soko la uhamisho, akifuatiwa na nyota wa Chelsea, Eden Hazard, halafu straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya tatu.
Namna gani CIES Football Observatory wamepata matokeo hayo?
Ili kupiga hesabu ya thamani ya uhamisho wa mchezaji yeyote, wametumia sababu mbalimbali za kisoka.
Sababu hizo ni pamoja na Umri wa mchezaji, mkataba wake wa sasa, nafasi anayocheza uwanjani, jumlisha matokea na mafanikio ya klabu yake.
Hapo chini ni graphics zinazoonesha sababu za kupata thamani ya uhamisho wa mchezaji:
Matokeo ya utafiti wao yanaonesha kuwa Lionel Messi ndiye mchezaji mwenye thamani kuwa zaidi kwenye soko la uhamisho akiwa na bei ya Euro milioni 255.3-280.8.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard ameshika nafasi ya pili akiwa na thamani ya Euro milioni 135.4-148.9.
Cristiano Ronaldo, ameshika namba tatu akiwa na thamani ya Euro milioni 113.3-124.7.
Ukiachana na Ronaldo ambaye amefikisha miaka 30, wachezaji sita tu wenye umri huo wameingia kwenye orodha ya wachezaji 100 ambao ni Yaya Toure, Santi Cazorla, Andrés Iniesta, Carlos Tevez, Thiago Silva na Luiz Fernandinho.
Matokeo hayo pia yanaonesha, Raheem Sterling wa Liverpool ameshika namba sita kwa kuwa na thamani kubwa kwenye soka la uhamisho, wakati mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane anashika nafasi ya 15.
Tazama Orodha nzima hapo chini:
0 comments:
Post a Comment