Singano aliyepiga magoti kusujudu bado anaipenda Simba
MASHABIKI wa Yanga jana walifurika uwanja wa Karume kushuhudia mazoezi ya timu yao, lakini walipomuona Ramadhan Singano ‘Messi’ akiingia kwenye Ofsi za Shirikisho la soka
Tanzania jana akiwa na gari aina ya Mazda kwa ajili ya kikao cha kujadili utata
wa mkataba wake na klabu ya Simba, walimshangalia na baadaye kuchangishana pesa
walizompatia wakijigamba kuwa Simba haina hela za kumpa, hivyo ajiunge na Yanga.
Ulikuwa utani wa jadi, lakini
kitendo hicho kimetafsiriwa tofauti na wadau wengi na kumezuka tetesi kuwa
kiungo huyo mshambaliaji amejiunga na mabingwa wa Tanzania bara, Young
Africans.
Kutokana na taarifa hizo,
Singano amekiri kupokea simu nyingi zikimuuliza kama kweli kajiunga na Yanga, lakini amekanusha uvumi huo.
Kupitia kwenye ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa facebook unaokwenda kwa jina la Ramadhan Singano
Messi amekanusa taarifa hizo na ameandika hivi:
0 comments:
Post a Comment