Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
UONGOZI wa Yanga umeapa kutosajili wachezaji kutoka kwa wapinzani wao wa jadi, Simba.
Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, amesema hayo jana wakati klabu hiyo inamtambulisha rasmi winga wao Malimi Busungu.
Muro amesema uongozi mpya wa Yanga hauko tayari kusajili nyota kutoka Simba kutokana na kasoro zilizojitokeza.
"Tumekuwa tukilaumika kwa wapenzi, wanachama na mashabiki wetu kutokana na kusajili nyota wa Simba. Leo (jana) Juni Mosi, 2015 mimi msemaji pekee wa Yanga Tanzania ninasema kwamba kamwe uongozi wetu hautasajili mchezaji kutoka Simba tena," amesema Muro.
Katika miaka ya karibuni Yanga imeshindwa kuifunga Simba huku baadhi ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo ya Jangwani wakiamini kuwa kuchemsha kwao kumetokana na kusajili wachezaji wanaotoka kwa wapinzani wao.
0 comments:
Post a Comment