Monday, June 1, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam


'Busungu amefanya kazi kubwa kuhakikisha Mgambo haiporomoki daraja msimu uliopita akifunga mabao 10.'

BAADA ya kutambulishwa rasmi akiwa mchezaji mpya wa nne wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Busungu amefunguka kilichomfanya atue katika klabu hiyoya Jangwani.

Busungu, winga wa kushoto aliyeng'ara na kikosi cha kocha mzawa Bakari Shime cha Mgambo Shooting Stars, alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akiwa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Kabuku, Handeni jijini Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa rasmi leo kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga jijini hapa, Busungu amesema sababu ya kuntu ya kujiunga bna Yanga msimu huu ni ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

Yanga, mabingwa mara 25 wa Tanzania Bara, wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani baada ya kuibuka mabingwa wa VPL 2014/15.

Busungu amewashukuru viongozi na wachezaji wa Mgambo kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichokuwa na klabu hiyo Kabuku, Tanga.

“Ninashukuru pia Yanga kwa kuona kipaji changu. Nimefurahi kwa sababu nitacheza katika timu inayoshiriki mashindano ya kimataifa, nimejipanga na niko tayari kwa mapambano,” amesema Busungu aliyekuwa amefuatana na meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Sale.

"Yanga ni timu kubwa ambayo mwakani itaiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa, ninaamini kila mchezaji anatamani kuwa sehemu ya kikosi chake," amsema zaidi Busungu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video