Huu ni wakati wa likizo kwa wachezaji wa timu za ulaya na kwingingine duniani.
Wakiwa kwenye ligi kawaida huwa hawapati muda wa kujiachia kufanya mambo ya starehe sana hasa kulewa kupindukia.
Sasa muda wa likizo ndio muda wa fungulia mbwa, mchezaji wa Aston Villa, Jack Grealish amepigwa picha na mtu asiyejulikana akiwa chini hoi baada ya kupiga pombe nyingi.
Grealish ambae ana miaka 19 habari zake pamoja na picha zimesambaa sana mtandaoni na inasemekana kwamba klabu yake itakutana nae hivi karibuni kutokana na picha hizo.
Uongozi wa Villa umesema kwamba wanajua kwamba picha za mchezaji wao zinasambaa sana na washamuita kuwa na kikao nae. Kuhusu maamuzi ya kinidhamu yatabaki kuwa mambo ya ndani ya klabu hiyo.
Lakini baada ya muda Jack Greaish alitumia account yake ya twitter kukanusha kwamba sio yeye kwenye picha.
0 comments:
Post a Comment