Wayne Rooney
Roonney ni mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli ya kuvutia katika klabu yake na timu ya taifa. Mpaka sasa Rooney ana taji moja tu la Ligi ya mabingwa Ulaya, hali inayompelekea kuingia katika kundi hili.
Eden Hazard
Hazard ana uwezo mkubwa sana wa kumiliki mpira, pia ana kasi na mwepesi wakati linapokuja suala la kufunga na kutoa pasi za magoli. Huyu ameingia katika kundi hili kutokana na kufananishwa na Christiano Ronaldo wakati akiwa Man United na pia akiwa na umri kama huu wa Hazard. Takwimu zinaeleza kuwa wastani wake wa kufunga magoli ni 0.25 tangu alipotua darajani mwaka 2012 huku Ronaldo akiwa na wastani wa 2.4 kwa mchezo wakati akiwa Manchester United kati ya miaka ya 2003 na 2009.
8. Jack Wilshere
Huyu anaonekana kuwa ni moja ya viungo bora klabuni Arsenal lakini ukiangalia kwa umakini hakuna kubwa aliliofanya klabuni hapo tangu alipoanza kupata nafasi timu ya wakubwa akitokea timu ya vijana.
7. Radamel Falcao
Huyu alikuwa ni mchezaji wa pili anayelipwa zaidi Manchester United baada ya kuja kwa mkopo akitokea Monaco, lakini kiwango chake duni kimesababisha United waachane naye. Amefunga magoli 4 katika michezo 26 aliyoichezea United msimu mzima uliopita.
6. David Luiz
Huyu ni beki aliyenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu ulimwenguni. Lakini kiwango chake katika timu ya Taifa hakiridhishi hali inayosababisha kuingia katika orodha hii.
5. Zlatan Ibrahimovic
Hakuna mtu anayeweza kulalamikia uwepo wake Ligi Kuu nchini Ufaransa,lakini je yuko vizuri kama ambavyo watu wengi wanavyofikiri?. Ukweli ni kwamba katika maisha yake yote ya soka Zlatan hajawahi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na haitazamiwi ni lini anaweza kushinda taji hilo kutokana na ukweli kwamba ligi aliyopo kwa sasa sio miongoni mwa ligi tatu bora barani Ulaya hivyo kuwa na fursa finyu ya kushinda taji hilo katika maisha yake ya soka.
4. Steven Gerrard
Hakuna mtu asiyetambua ubora wake katika ulimwengu wa soka, lakini kutopata mafanikio ya kutosha katika klabu yake kumemfanya aingie katika orodha hii ya wachezaji wanaopewa sifa kubwa kuzidi walichokifanya katika ulimwengu wa soka.
3. Mario Balotelli
Yamkini huyu ndio mchezaji aliyeonesha kiwango kibovu kabisa msimu ulimalizika wa ligi kuu nchini Uingereza hasa ukilinganisha na jina lake linavyotamkwa vinywaji mwa wapenda soka ulimwenguni. Akiwa na klabu ya Liverpool msimu huu amefunga goli moja tu EPL na hivyo thamani yake haiendani na anachokifanya uwanjani. Huyu amekamata nafasi ya tatu katika orodha hii.
2. Nicolas Anelka
Huyu anajulikana kama moja ya wachezaji wachezaji ambao wamewahi kuvichezea vilabu vingi sana katika maisha yake ya soka. Mwaka 2013 ilikuwa bado kidogo tu astaafu soka lakini cha kushangaza alipewa mkataba na klabu ya West Bromwhich huku ikifahamika wazi kuwa alikuwa hana la ziada katika soka. Kwa sasa anakipiga katika klabu ya Mumbai City FC huko nchini india.
Gareth Bale
Huyu ndiye mchezaji ghali kuliko wote duniani kwa sasa lakini kiwango chake uwanjani hakilingani na thamani ya Euro miliono 100 ambayo ndio kiasi alichonunuliwa kutoka Tottenham. Tangu mwka 2013, Bale amefunga magoli 33 na kutoa pasi za magoli 22 huku akiachwa mbali na Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli 112 na Karim Banzema magoli 46 ambao walinunuliwa kwa Euro milioni 80 na 41. Msimu uliopita Bale amefunga magoli 11 tu.
Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa sokkaa.com
0 comments:
Post a Comment