Wakati wanaripoti mechi ya nusu fainali ya Copa America kati ya Chile na Peru usiku wa kuamkia leo, kituo cha runinga cha Colombia kimethibitisha kwamba Radamel Falcao amesaini mkataba Chelsea.
Dili la Falcao kujiunga na Chelsea limekuwa likiripotiwa wiki chache zilizopita na Jose Mourinho anakusudia kurudisha makali ya straika huyo aliyepewa jina la "El Tigre" kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu enzi hizo akiwa Atletico Madrid.
Katika show ya TV ya Colombia inayoitwa Gol Caracol, mwandishi wa habari, Javier Herndandez amethibitisha kwamba Falaco amesaini mkataba Chelsea jana Jumatatu.
Bonett ameongeza kuwa Falcao atatambulishwa rasmi Julai 19 au 20 nchini Canada ambako Chelsea watakuwa wanafanya mazoezi.
The Blues watacheza na New York Bulls Julai 23 mwaka huu katika mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Hata hivyo mashabiki wengi wa Chelsea wanajiuliza kama kweli Falcao atawafaa hasa baada ya kuonesha kiwango kibovu katika michuano ya Copa America na hata alipokuwa Manchester United msimu uliopita.
Hebu msikilize Javier Hernandez Bonett akiripoti dili la Falcao kutua Chelsea...
0 comments:
Post a Comment