Boniface Wambura
BODI ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) imezitaka klabu za
ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuendana na kalenda ya usajili ambao mara
nyingi huleta usumbufu.
Afisa Mtendaji mkuu wa TPLB, Boniface Wambura Mgoyo amesema tayari TFF wametoa kalenda ya usajili
na kuanza kwa ligi kuu, hivyo klabu ziwape fursa makocha kusajili wachezaji
wanaowataka ndani ya muda uliotangazwa, wakati wao wanaendelea na maandalizi
mengine ikiwemo kukagua viwanja na kuzungumza na wadhamini.
“Maeneo mengine ambayo Bodi inafanyia kazi ni maandalizi ya kugagua
viwanja vitavyotumika. Vilevile kabla ya ligi kuanza tutakuwa na ‘Physical
fitness test’ na semina kwa waamuzi na makamishina. Amesema Wambura na
kusisitiza: “Pia tuna maandalizi ya wadhamini ambao tumeanza kuwasiliana nao
ili kukamilisha kila kitu mapema. Kwa upande wa Azam Media wanaendelea
kudhamini, tunawasiliana nao ili fungu la kwanza la fedha litoke kwa ajili ya
maandalizi ya timu”.
“Haya ni baadhi ya maeneo ambayo tunayafanyia
kazi, lakini tunasisitiza suala la usajili kwasababu linakuwa na matatizo.
Tunajua timu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza zinatumia usajili wa mtandao,
kuna timu zimepanda na zinahitaji mafunzo kwa ajili ya usajili wa mtandao, bila
shaka TFF wamejipanga kwa hilo”.
0 comments:
Post a Comment