Kiungo
mkongwe na mahiri wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, Andrea Pirlo
anatarajia kukutana na maofisa wa klabu ya soka ya Sidney, huku mwakilishi wa klabu hiyo akijaribu
kumshawishi kutua nchini Australia na kuachana na mpango wa kujiunga na New
York City inayoshiriki ligi ya soka nchini Marekani.
Kiungo
huyo mwenye miaka 36 hivi sasa, amepata kuiwakilisha timu yake ya taifa mara
113.
Pirlo
ambaye alishindwa kuisaidia timu yake kutamba mbele ya Barcelona katika mchezo
wa fainali ya klabu bingwa Ulaya jumamosi iliyopita wakichapwa mabao 3-1,
anahusishwa na kuihama klabu yake ya Juventus baada ya kubakiwa na msimu mmoja
tu katika mkataba wake.
Pamoja
na kuenea kwa taarifa za kiungo huyo kuhamia klabu anayoichezea kiungo wa
zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard, New York City ya nchini
Marekani, lakini mmoja wa mawakala wa
klabu ya Sidney ya nchini Australia amekaririwa akisema wanamhitaji mchezaji
huyo kwa udi na uvumba.
“kazi
yangu ni moja tu hapa nchini Italia. Kama Pirlo ataondoka hapa Turin, basi
nitamshawishi ajiunge na timu yetu ya Sidney” alisema afisa huyo na mwakalishi
wa klabu hiyo.
Wakala
huyo aitwaye Lou Sticca amethibitisha kuwa Sidney inahitaji mchezaji mkubwa ili
azibe mapengo yaliyoachwa wazi na wachezaji kadhaa nyota walioihama klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment