Licha ya Barcelona kuchukua ubingwa wa UEFA, bado thamani ya Brand yake sio kubwa zaidi ya klabu tano za juu yake.
Kwa mara ya kwanza Manchester United imevunja rekodi kwa kufikisha brand value ya zaidi ya Dola za Marekani bilioni moja na kuziacha brand nyingine zaidi ya dola millioni 300.
Namba mbili inakamatwa na wakali wa Bundesliga, Bayern Munich ambao brand yao ina thamani ya dola millioni 933 na mwaka jana ilikuwa namba moja.
Namba tatu imeenda kwa Real Madrid kwa kuwa na thamani ya dola millioni 873.
Vitu vya kuzingatia ni kwamba kwenye top 10 kuna brand 6 kutoka EPL ambazo ni Manchester united, Manchester city, Chelsea, Arsenal, Liverpool na Tottenham.
Licha ya Juventus kucheza fainali ya UEFA lakini kwenye brand value hata top 10 haipo kwasababu imeshika namba 11.
List kamili hii hapa
![list](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/06/list.jpg)
![list 1](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/06/list-1.jpg)
0 comments:
Post a Comment