Wednesday, June 3, 2015



*Yasema haitapokea usajili wa wachezaji wapya
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezionya kiana klabu kongwe za soka nchini, Simba na Yanga baada ya kuweka wazi kwamba halitaidhinisha usajili wa wachezaji wapya wa klabu ambazo zimeshindwa kuwalipa nyota waliowahi kuzitumikia.

Katibu mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, aliyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha Sports Bar cha Clouds TV, ikiwa ni muda mfupi baada ya kurejea kutoka Zurich, Uswisi alikokuwa amehudhuria mkutano mkuu wa uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

"Itafikia kipindi Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF haitapitisha usajili wa wachezaji wapya wa klabui ambazo bado hazijawalipa wachezaji ambao waliwahi kuzitumikia.

"Maana unakwendaje kuona mke wa pili wakati mke wako wa kwanza umeshindwa kumtimizia mahitaji kiasi cha kufikia hatua ya kuzunguka mitaani kusaka mahitaji muhimu," alisema Mwesigwa.

Ingawa hakuweka wazi klabu ambazo alikuwa anazilenga, kauli ya Mwesigwa ni kama onyo kwa klabu kongwe nchini, Simba na Yanga ambazo zimekuwa na tabia ya kuwaacha wachezaji pasipo kuwatimizia mahitaji yao.

Februari 4 mwaka huu FIFA iliipa Simba siku 30 kuhakikisha inamlipa aliyekuwa beki wake wa kati Donald Mosoti dola za Marekani 13,800 (Sh. milioni 27.6) kutokana na kusitisha mkataba wa Mkenya huyo.

Katika barua yake kwa TFF iliyokuwa na anuani ya FAX +4143/222 77 55, FIFA iliagiza Simba kumlipa Mosoti ndani ya muda huo dola 13,800 na penalti ya asilimia tano (5%) ambayo ni dola za Marekani 600 kutokana na kumharibia mipango yake kisoka kuanzia Desemba 12, 2013 walipomtimua hadi siku ambayo malipo yatafanyika.

Mbali na kuvunja mikataba ya Waganda Danny Sserunkuma na Simon Sserrunkuma mara tu baada ya kumalizika msimu uliopita, Simba pia inadaiwa dola la Marekani 17 (Sh. milioni 34) na mfungaji bora wa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2013/14, Amissi Tambwe kutokana na klabu hiyo ya Msimbazi kuvunja mkataba na Mrundi huyo Desemba 14 mwaka jana.

Yanga pia ilishawahi kuagizwa na FIFA kumlipa beki wa kushoto John Njoroge Sh. million moja za Kenya (Sh. milioni 10 za Tanzania) baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuvunja makataba wake kienyeji.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video