Tuesday, June 30, 2015

Chelsea wametoa dau la pauni milioni 6 kumtaka kipa Asmir Begovic, 28, kuziba nafasi ya Petr Cech, 33 aliyehamia Arsenal (Telegraph).
Tottenham huenda wakamtoa Emmanuel Adebayor, 31 kwenda Aston Villa kubadilishana na Christian Benteke, 24 (Daily Mirror).
West Ham huenda wakamtaka mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 24, lakini Liverpool huenda wakamtumia kumwania Benteke (Independent).
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anakaribia kukamilisha usajili wa wachezaji watatu, Nathaniel Clyne, 24, kutoka Southampton, Bobby Adekanye, 16 kutoka Barcelona na Ludwig Augustinsson, 21 kutoka FC Copenhagen (Daily Star).
Manchester City wanafikiria kumchukua beki kutoka Brazil Fabinho, 21 anayechezea Monaco (Daily Mail).
Baada ya kumkosa Bastian Scheinsteiger Manchester United watajaribu kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, 25 (Daily Express).
Douglas Costa wa Shakhtar Donestk amesema Bayern Munich wanamtaka (Guardian).
Arsenal wameacha kumfuatilia kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 28 (Telegraph).
Badala yake Arsene Wenger angependa kumchukua kiungo wa Sporting William Carvahlo, 23 (London Evening Standard).
Everton wanamfikiria beki wa kulia wa Leeds United Sam Ryram, 21, wakati Manchester United wakifikiria kumchukua Seamus Coleman 26 (Daily Express).
Meneja mpya wa West Ham Slaven Blic ametakiwa kumaliza katika nafasi nane za juu na atafukuzwa kazi bila fidia kama klabu hiyo itashuka daraja (Sun).
West Ham wanajaribu kumsajili beki wa kati kutoka Tunisia Aymen Abdennour, 25 kutoka Monaco na Alex Song, 27 kutoka Barcelona (Daily Mail).
Meneja wa manchester United Louis van Gaal amemuambia kipa David De Gea, anayesakwa na Real Madrid, kuripoti kambini siku ya Jumatatu (Daily Star). Kiungo kutoka Uturuki Arda Turan, 28, anajiandaa kuondoka Atletico Madrid na atatangaza anakwenda wapi siku chache zijazo, kwa mujibu wa wakala wake. Mchezaji huyo anatakiwa na Barcelona, Paris St-Germain na Manchester United (NTVSpor).
West Brom wanataka kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kumchukua Charlie Austin, 25 anayeuzwa kwa pauni milioni 15 (Birmingham Mail).
Barcelona wametoa dau la euro milioni 80 na nyongeza nyingine milioni 10 kumtaka Paul Pogba. Chelsea wametoa euro milioni 50 pamoja na Oscar, huku Manchester City wakitoa euro milioni 100 (Sport).
Juventus wangependa kumuuza Pogba kwenda Barcelona kwa sababu Pogba ataendelea kuichezea klabu yake kwa kuwa Barca wana kikwazo cha kusajili hadi msimu ujao (Sport).
Arsenal watawapa napoli pauni milioni 9 kutaka kumsajili Faouzi Ghoulam, 24 wiki hii. Mchezaji huyo pia anatazamwa na Chelsea na Manchester City, lakini Arsenal wana nafasi kubwa ya kumchukua (Metro).
Manchester United wametoa euro milioni 40 kumtaka Sergio Ramos wa Real Madrid (Sky Sports).
Chelsea wanajiandaa kupanda dau kumtaka beki wa Everton John Stones anayethamanishwa kwa pauni milioni 20 (Daily Express) na AC Milan wanataka kumchukua kiungo wa Tottenham Erik Lamela wakishindwa kumsajili Axel Witsel (Mediaset).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video