Beki wa kulia wa England, Nathaniel Clyne, 24, atakamilisha uhamisho wa pauni milioni 12.5 kutoka Southampton kwenda Liverpool (Liverpool Echo), Manchester City wameungana na mahasimu wao Manchester United kutaka kumsajili beki wa Real Madrid Serrgio Ramos, 29 (Mirror), kiungo wa Juventus Artruro Vidal, 28, anaonekana kujiandaa kuhamia Arsenal msimu huu (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 24, anajiandaa kuhamia West Ham kwa pauni milioni 8 (Daily Telegraph), Manchester United watatoa dau jingine la pili kumtaka Sergio Ramos baada ya dau la kwanza la pauni milioni 28.3 kukataliwa (Manchester Evening News), kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ameonesha kutaka kumsajili Oscar 23, kutoka Chelsea (London Evening News), Chelsea ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomuwania kiungo mshambuliaji wa Atletico Madrid Arda Turan, 28, huku wakala wake akisema anazungumza na "vilabu vitatu au vinne" (Daly Mail), Newcastle United wanataka kumsajili winga wa West Ham Stewart Downing, 30, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Sunderland na Leicester City (Daily Express), ahadi ya kuweza kuwepo katika kikosi cha kwanza cha Man Utd huenda ikamvutia Bastian Schweinsteiger, 30, kwenda Old Trafford (Times), kipa wa zamani wa Man Utd Peter Schmeichel amemtaka David De Gea, 24, kukataa kwenda Real Madrid na kubakia kuwa nguli wa United (Sun), Erik Lamela wa Tottenham anazungumza na angalau klabu moja ya Italia na inadhaniwa kuwa Juventus (Mirror), Liverpool wamepanda dau jipya kumtaka kiungo Asier Illarramendi, 25, baada ya dau lao la awali la pauni milioni 10.6 kukataliwa (Daily Star), Everton wanasema beki wao wa kulia Seamus Coleman, 26, ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester United, hauzwi (Liverpool Echo), Arsenal wangeweza kushinda EPL msimu uliopita kama wangefundishwa na Jose Mourinho, kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Tony Cascarino (Sky Sports), Newcastle wanataka kumchukua beki wa Schalke Joel Matip, 23, lakini wamebadili mawazo ya kumtaka Ron Vlaar, 30, wa Aston Villa (Newcastle Chronicle), mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba, 30, amekataa kwenda West Brom na badala yake atajiunga na Shanghai Shenhua ya China kwa pauni milioni 11 akitokea Besitkas (Guardian). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!
Monday, June 29, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment