Wednesday, June 3, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Tenga ameliongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa mafanikio makubwa akiwa Rais wa shirikisho hilo anayesifika kwa utawala bora.'
MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga, ameiomba serikali ya Tanzania kuwekeza kikamilifu katika sekta ya michezo.
Tenga (59) ameyasema hayo jijini hapa leo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lipate uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katika hafla hiyo, Tenga amekabidhiwa vyeti viwili vya kutambua mchango wake katika soka la Tanzania. Cheti cha kwanza kikiwa ni cha timu nzima ya taifa (Taifa Stars) ya 1979-1980 iliyofuzu kwa mara ya Fainali za Afrika nchini Nigeria na cha pili kilikuwa cha kuwa miongoni mwa Marais wa TFF.
Baada ya kukabidhiwa cheti cha Stars ya 1979-1980 aliyokuwa nahodha, Tenga amesema: "Hiki cheti ndicho chenyewe. Nimefurahi sana. Sasa ninaiomba serikali yetu iwekeze 'seriously' (kimalifu) katika michezo ili kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta hii."
Nyota huyo wa zamani wa Pan Africans pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video