Je, safu kali ya ushambuliaji ya Falcao na Diego Costa itarudi tena Chelsea?
Wawili hao wakiwa Atletico Madrid kwa msimu mmoja (2012/2013), kocha Diego Simeone aliwatengeneza kuwa washambuliaji hatari zaidi barani ulaya.
Kitu cha kukumbukwa zaidi ni namna walivyoichachafya Real Madrid kwenye fainali ya Copa del Rey.
Wakati huo Costa alikuwa amerejea klabuni hapo kutokea kwenye maisha ya kucheza kwa mkopo na alipoungana na Falcao, walionesha cheche kali.
Falcao alikuwa straika wa kuogopwa mno na mabeki mpaka ikifikia watu kumuita El Tigre.
Kipindi wanacheza wote Atletico, nyota hao walikuwa wanafunga magoli katika kila mechi kwa wastani wa 1.8
Mashabiki wa Chelsea wamepokea vibaya taarifa za Falcao kutua Stamford Bridge, lakini wakumbuke kuwa kitendo cha kuungana na Costa kinaweza kumfanya arudishe makali ya zamani kwani wanajuana vizuri.
Tazama takwimu za kuvutia za Falcao kutoka katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.

0 comments:
Post a Comment