Ikiwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imekwishawasili nchini Misri kuvaana na timu ya Taifa ya Misri kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya
Africa (AFCON) 2017, itamkosa mshambuliaji wake, Mrisho Ngasa katika mechi hiyo
ya kesho.
Ngasa ambaye ataikosa mechi hiyo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, nafasi yake itazibwa na Amri Kiemba,
ambaye ameondoka hiyo jana hadi mjini Cairo ambako ameungana na Stars.
Stars iliweka kambi yake ya wiki
moja nchini Ethiopia kujifua tayari kuikabili Misri siku ya jumapili.
0 comments:
Post a Comment