WACHEZAJI wawili wa kimataifa wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho na Mliberia, Kpah Sherman wanatua leo jijini Dar es salaam kujiunga na wenzao walioanza mazoezi jumatatu ya wiki hii kujiwinda na ligi kuu msimu ujao, michuano ya Kagame na klabu bingwa barani Afrika.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amesema kwamba wachezaji hao ni mali ya Yanga na wanakuja kuanza maandalizi ya Kagame.
Tiboroha amesema wanandinga hao wawili walitarajiwa kuwasili jana, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao walishindwa kusafiri na wanaingia leo panapo majaaliwa kwani wote wapo safarini.
Imefahamika kwamba Coutinho alishindwa kusafiri kutokana na hali mbaya ya hewa angani, wakati tiketi ya Sherman ilikuwa na tatizo, lakini kila kitu kimewekwa sawa.
0 comments:
Post a Comment