MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda aliyechemsha Simba na kutemwa, Dan Sserunkuma yuko mbioni kurejea katika klabu iliyomfanya ang'are katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL) - Nairobi City Stars.
Hii imethibitishwa na mwenyekiti wa klabu, Peter Obuya ambaye ameeleza kuwa kila kitu kitamalizwa leo Jumatatu Juni 29, 2015.
“Tumefikia makubaliano na kumsajili tena Sserunkuma kwa mkataba wa mwaka mmoja. Tumejadili kila kitu kuhusu kurejea kwake na maslahi yake pia. Tutamtambulisha Jumatatu ikiwa jambo dogo lililobaki, litamalizwa mapema. Kwa sasa tuko katika hatua nzuri," amesema.
Kukamilika kwa dili hilo kutafuta minong'ono na taarifa zinazodai kuwa mshambuliaji huyo alikuwa anataka kurejea Gor Mahia aliyolipa taji la msimu uliopita huku akiibuka mfungaji bora kwa kuziona nyavu mara 16.
City Stars ilikuwa timu ya kwanza kwa Sserunkuma kuitumikia KPL 2011 baada ya kuachana na Victors FC na baadaye kusajiliwa kwa fedha nyingi Gor Mahia Januari 2012.
0 comments:
Post a Comment