MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na sasa JKT Ruvu, Betram
Mwombeki ameamua kuachana na soka na kurejea kwenye fani yake ya zamani ya
uvuvi na ufugaji.
Mwombe amekaririwa na E-fm usiku huu akisema kwasasa yuko
Mwanza kwa mapumziko na muda si mrefu anaanza shughuli za ya kufuga na kuvua
samaki kwasababu anasumbuliwa sana na miguu inayomuuma kwenye unyayo.
“Niko Mwanza sasa hivi, nimeamua kuachana na mpira kwasababu
naumwa miguu kwa chini, kama nachomwa sindano vile. Ilianza niliposajiliwa JKT
Ruvu, lakini nikiwa Simba haikuwa kunitokea”. Amesema Mwombeki na kuongeza: “Nimeamua
kurudi kwenye fani yangu ya zamani ya ufugaji na uvuvi”.
Mwamboki amebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yake
ya JKT Ruvu, lakini anaamini watamalizana bila matatizo yoyote.
0 comments:
Post a Comment