Ame Ally 'Zungu' aliyesajiliwa na Azam FC akitokea Mtibwa Sugar, leo ameanza rasmi mazoezi na kikosi chake hicho kipya kilichomkabidhi jezi namba 24 iliyokuwa ikivaliwa na Gaudence Mwaikimba aliyejiunga na JKT Ruvu.
Ame ameungana na wenzake na kupiga matizi kujiandaa na mashindano ya kombe la Kagame. Jezi hiyo ndiyo atakayochezea michuano mbalimbali watakayoshiriki, lakini akatamka maneno mazito sana.
Mchezaji huyo ambaye ni mshambuliaji, amesema ana kila sababu ya kujituma kwa nguvu zote ili Azam ifanikiwe na hakuna kisingizio kwa sababu kila kitu anachotakiwa awenacho mchezaji wa kisasa kipo.
“Azam hii kweli ni profesheno, kuna kila kitu ambacho mchezaji wa kisasa anatakiwa kuwa nacho, gym, bwawa la kuogelea, viwanja yaani mchezaji ushindwe mwenyewe,”alisema Ame.
“Hivyo, nina kila sababu ya kufanya vizuri kuhakikisha Azam inasonga na isijutuie uamuzi
Chanzo: Tovuti ya Azam FC.
0 comments:
Post a Comment