Kwa mujibu wa
taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa
amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa.
Pistorius alikuwa
amefungwa mwaka uliopita kati kesi iliyovutia hisia kali kutoka kote duniani.
Kiongozi wa Mashtaka
Gerrie Nel alidai kuwa Pistorius alimpiga risasi na kumuua bi Steenkamp baada
ya wawili hao kuzozana.
Kiongozi wa Mashtaka
amekata rufaa ya kuachiliwa kwake na mahakama kuu ya rufaa imeratibiwa kuanza
kusikiza kesi hiyo mwezi Novemba.
Bwana Nel anaitaka
mahakama hii kumuongezea Pistorius kifungo japokuwa mmoja wa jamaa zake
Pistorius amedai kuwa mwanariadhaa huyo atasamehewa kabla ya mwisho wa Agosti
mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment