MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka ya kulipwa katika Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mbwana Samatta, amesema timu ya Taifa, Taifa Stars inamuumiza mno kichwa.
Taifa Stars imeweka kambi ya wiki moja mjini Addis Ababa, Ethiopia kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Misri wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zilizopangwa kufanyika mwakani nchini Gabon.
Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam kabla ya Taifa Stars kwenda Addis Ababa, Samatta alisema timu hiyo inamweka katika wakati mgumu kutokana na hakuna jambo nzuri aliloifanyia.
Samatta alisema malengo yake hayajatimia kwa Taifa Stars kwani hajaweza kuifikisha kule Watanzania wanahitaji ikiwa ni kuiona inafuzu michuano ya Afrika na mengine.
0 comments:
Post a Comment