Sunday, June 14, 2015

Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba mbele ya Mafarao, timu ya taifa ya Misri baada ya kukubali kipigo cha goli 3-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Africa (AFCON), michuano ambayo itafanyika nchini Gabon mwaka 2017.
Stars iliweza kuhimili mikikimikiki ya Mafarao hao kwa kipindi chote cha kwanza lakini balaa lilianza kipindi cha pili ambapo Rami Rabia aliiandikia Misri bao la kwanza dakika ya 61, takribani dakika nne tu tangu Stars iliporuhusu bao la kwanza, ilijikuta ikiruhusu goli la pili baada ya Basem Morsi kuifungia Misri goli la pili mnamo dakika ya 65 ya mchezo. 
Mambo yalizidi kuwaendea kombo Stars mara baada ya Mohamed Salah kushindilia msumari wa mwisho mnamo dakika ya 70 na kumaliza kabisa mipango ya Stars kwenye mchezo huo.
Taifa Stars ilionekana kuzidiwa hasa kipindi cha pili ambapo muda mwingi ilikuwa ikishambuliwa na Wamisri walioonekana kuwa na njaa ya ushindi kwa muda wote wa mchezo kutokana na kutopata goli kwenye kipindi cha kwanza.
Stars itakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi lake kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza na hali inaonekana kuwa mbaya zaidi kutokana na aina ya timu ambazo imepangwa nazo kwenye kundi moja. 
Mbali na Misri, Stars ipo kundi moja na Nigeria pamoja Chad.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video