Wednesday, June 10, 2015

SPUTANZA leo inapeleka malalamiko yake tena kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu uamuzi uliotolewa jana kuhusu mgogoro uliopo kati ya Simba SC na Ramadhani Singano ‘Messi’.
 SPUTANZA imefikia uamuzi huo baada ya kutafakari uamuzi uliotolewa na TFF na kuona bado kuna mapungufu ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa utata unaoweza kujitokeza kati ya pande hizo mbili.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wachezaji Soka Tanzania (SPUTANZA) Mussa Kisoky amesema, uamuzi uliotolewa jana na TFF kwamba Singano anatakiwa kufanya mazungumzo na kukubaliana upya na ‘Wekundu wa Msimbazi’ bila kusema kama mchezaji huyo yupo huru kufanya mazungumzo na timu nyingine bado haitoshi hasa pale kama wawili hao hawatafikia makubaliano.
“Sisi hatukubaliani na maamuzi yale yaliyofikiwa jana kutokana na kikao cha kawaida kilichoitishwa na TFF ndio maana wakasema kama mikataba ile ina matatizo  wazikutanishe pande hizi mbili ziweze kukubaliana kwenye makubaliano mapya ya mkataba, kwahiyo kwetu sisi hicho kiu siyo kibaya sana ni mwanzo mzuri”, amesema Kisoky.
“Lakini hata hivyo sisi kwa upande wetu tumekaa usiku na kutafakari tumeona bado haijatosheleza, leo nitakuwa na nafasi ya kwenda kukutana na hao wakubwa tena, tunataka kila kitu kiwekwe wazi”, Kisoky amefafanua.
“Mimi sipo peke yangu, kuna katibu mkuu, katibu msaidizi, kuna yeye Singano, kuna jamaa zake na ndugu, katika kukaa ‘as a team’ tumeona bado kuna suala jingine ambalo limejificha ndani yake ambalo halitaleta kitu kizuri kwa maana moja. Messi na Simba watakaa kukubaliana makubaliano mapya, je wasipokubaliana itakuwaje? Je sasa hivi kwa kusema wafanye makubaliano mapya Messi yupo huru? Tunaomba ufafanuzi zaidi”, amesema.
“Pia kuna barua yetu tuliiwasilisha Simba wiki iliyopita ambayo ina madai mapya, tunataka ifanyiwe kazi, kwa maana Simba walishavunja mkataba kikatiba na Messi. Kuna vipengele vinasema vitalipa baadhi ya vitu lakini toka amesaini Messi hajawahi kutekelezewa kwa vipengele hivyo, kuna kipengele cha bima tunaamini kila mchezaji anapaswa kuwa na bima kama sheria ya soka inavyosema. Kuna kipengele wao wenyewe wameji-commit kumpa Messi pesa za nyumba na kipengele cha tiba, kuna kipengele cha asilimia 25 kama akiitwa kwenye national team kwahiyo hivyo vitu tuliviwasilisha kabla hata ya maamuzi yao”, ameongeza.
Jana jioni TFF iliamua kuwa, Simba na Singano wakae pamoja na kujadiliana kuona kama wanaweza wakapata suluhu ya mgogoro wa kimkataba unaowakabili lakini haikuweka wazi kwamba Singano ni mchezaji huru na kama anaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote mbali na Simba.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video