Klabu ya ‘Wekundu wa Mimbazi’ Simba imesema inatarajia kumsanisha mkataba mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Uganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ ili kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema, kuna mtu alikuwa anashughulikia suala hilo na kila kitu kimekwenda vizuri kilichobaki ni makubaliano ya mshahara wa mkali huyo na mambo mengine madogomadogo ili aweze kumwaga wino kujiunga na vijana wa Msimbazi.
“Kuna mtu alikuwa anashughulikia hilo suala lakini nafikiri yamebaki mambo madogo sana, tumeamua kumchukua Kiiza ili aongeze nguvu pale kwenye ‘striking force’”, amesema Poppe.
“Kama walishafikia makubaliano basi kilichobaki ni kusaini mkataba, makubaliano kwamba ni kiasi gani cha mshahara atalipwa, mambo ya marupurupu na vitu kama hivyo tukikubaliana hapo atasaini mkataba”, ameeleza.
“Kunawachezaji wengine wawili mmoja midfielder mwingine striker nafikiri kufikia kesho au keshokutwa tutawapa habari zake kamimili”, alimaliza.
Klabu ya ‘Wekundu wa Mimbazi’ Simba imesema inatarajia kumsanisha mkataba mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Uganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ ili kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema, kuna mtu alikuwa nashughulikia suala hilo na kila kitu kimekwenda vizuri kilichobaki ni makubaliano ya mshahara wa mkali huyo na mambo mengine madogomadogo ili aweze kumwaga wino kujiunga na vijana wa Msimbazi.
“Kuna mtu alikuwa anashughulikia hilo suala lakini nafikiri yamebaki mambo madogo sana, tumeamua kumchukua Kiiza ili aongeze nguvu pale kwenye ‘striking force’”, amesema Poppe.
“Kama walishafikia makubaliano basi kilichobaki ni kusaini mkataba, makubaliano kwamba ni kiasi gani cha mshahara atalipwa, mambo ya marupurupu na vitu kama hivyo tukikubaliana hapo atasaini mkataba”, ameeleza.
“Kunawachezaji wengine wawili mmoja midfielder mwingine striker nafikiri kufikia kesho au keshokutwa tutawapa habari zake kamimili”, alimaliza.
0 comments:
Post a Comment