SAA chache baada ya TFF kutoa taarifa kwamba Singano na
Simba wanatakiwa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya wa msimu mpya wa 2015/16, baada
pande zote kueleza kutambua utata ulio
ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa
sasa wa Simba SC, mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Hajji Manara
ameibuka na kusema kamati ya utendaji ya klabu hiyo inakutana kesho kujadili
suala hilo.
“Kamati ya utendaji ya Simba, kesho jioni inakutana kujadili, pamoja na mambo mengine tutajadili
sakata la Singano, tutajadili mapendekezo ya TFF na kutoa majibu” Manara
amekaririwa na E-fm usiku huu.
Hata hivyo katika kikao hicho, uongozi wa Simba uliwakilishwa
na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin
Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano aliandamana na Uongozi wa Chama cha
Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA).
Kutokana na kauli ya Manara haijafahamika Simba
inakwenda kujadili nini juu ya mkataba wa Singano kwasababu nao walikuwepo
kwenye kikao hicho na Collins ameweka saini makubaliano hayo, labda kama amelazimishwa
na TFF kufikia maamuzi ya kuifuta
mikataba yote miwili yenye utata.
0 comments:
Post a Comment