WEKUNDU wa Msimbazi, Simba hawana uhakika wa kushiriki
michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama kombe la Kagame
inayoanza kutimua vumbi jijini Dar es salaam Julai 11 mwaka huu.
Awali makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Erick Nyange ‘Kaburu’
alisema watashiriki michuano hiyo sawasawa na kauli iliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu mkuu, Selestine
Mwesigwa kwamba wameichagua Simba badala
ya Mbeya City fc wenye uhalali wa kupata nafasi hiyo.
Mwesigwa aliyekaririwa na Mtandao huu alisema Simba wana
heshima kubwa, wamekuwa mabingwa mara nyingi wa Kombe la Kagame, hivyo hawawezi
kuwatoa.
Lakini leo hii mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe amesema hana uhakika kama watashiriki Kagame kwani mpaka
sasa hawana mwaliko rasmi kutoka baraza la soka Afrika mashariki na kati,
CECAFA.
“Sidhani kama tutacheza, timu yenyewe hatujaipanga kuanza
mazoezi. Hatuwezi kupeleka timu ambayo haijatayarishwa. Kama mpaka sasa
hatujapewa mwaliko rasmi, inakuwa tatizo kuanza mazoezi. kama unavyojua kuna
wachezaji wengi wapo timu ya taifa, hatuwezi kuingia kwenye mashindano makubwa
kama haya kienyeji-enyeji”. Amesema Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment