Sergio Ramos amewaambia Real Madrid kwamba anataka kujiunga na Manchester United majira haya ya kiangazi.
Mwishoni mwa Juma lililopita, United walianza kwa kuweka mezani dau la paundi milioni 28.3 ili kuinasa saini ya nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, lakini Madrid walichomoa.
Hata hivyo, baada ya kuambiwa huhusu ofa hiyo, Ramos ameweka wazi kwa Real Madrid kuwa wanatakiwa kukaa na United na kufikia makubaliano juu ya uhamisho wake wa kutua Old Trafford.
Taarifa hizo zimewashitua Madrid ambao walitarajia kumaliza suala la mkataba wake, lakini sasa wamechanganyikiwa kwani dalili zinaonesha jamaa anasepa.
0 comments:
Post a Comment