BAADA ya Ramadhan Singano ‘Messi’ na Simba kukubaliana kuanza
mazungumzo ya makubaliano mapya ya mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa
2015/16 kufuatia pande zote kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo
ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC, Wekundu wa Msimbazi bado wanahitaji
kulijadili sakata hilo katika kikao cha kamati ya utendaji kitakachoketi leo.
Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema kikao
hicho kina agenda nyingi ikiwemo sakata la Singano na wanalijadili kwasababu
halijaisha kama watu wengi wanavyodhani.
“Mimi nilikuwepo wakati Mwesigwa (Selestine) akitoa taarifa
hii ya maazimio ya kikao na bahati nzuri kwenye kikao tulikuwa na mjumbe wa
kamati ya utendaji bwana Collins (Frisch), naamini kikao kilienda vizuri”. Amesema
Manara na kuongeza: “Nilichosikia katibu mkuu Mwesigwa akisema ni kwamba katika
kipindi hiki, si vizuri pande zote mbili tukalizungumza hili jambo, namimi
naheshimu sana mamlaka hizi. Unajua katika hali ya kawaida, ile kauli ilikuwa
inanilenga mimi na inamlenga Singano na wawakilishi wake”.
“Lakini baada ya kile kikao nimezungumza na Rais wa klabu
(Evans Aveva), nimezungumza na viongozi wa klabu, kesho (leo) kamati ya
utendaji ya Simba inakutana, pamoja na kujadili mambo mengine yahusuyo klabu,
tutalijadili jambo la Messi kwa mapana yake na kisha tutatoa maamuzi”.
Hata hivyo Manara amefafanua kuwa katika kikao hicho Singano
hatakuwepo kwasababu si mjumbe wa kamati ya utendaji.
“Mchezaji Ramadhan Yahya Singano si mjumbe wa kamati ya
utendaji, kikao hiki hakina agenda moja, ila agenda mojawapo itakuwa ni hii
ishu ya Singano. Simba inayo haki na
kukaa, kwasababu kule tulikuwa na mwakilishi (Collins) lazima alete mrejesho wa
kikao kwenye kamati ya utendaji na baadaye kamati itasema inachukuliaje mapendekezo
ya TFF, kama ni kuridhia na kukaa na mchezaji ili kuzungumza naye au kivyovyote
vile, jambo hili halijaisha kama watu wengi wanavyofikri”. Amesema Manara.
0 comments:
Post a Comment