Saturday, June 13, 2015

David Faramola Oniya

BEKI wa Nigeria,  David Faramola Oniya mwenye miaka 30 amefariki dunia leo baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki baina ya klabu ya Malaysia Club T-Team na Kelantan.
Vyombo vya habari vya Malaysia vinaeleza kwamba nahodha huyo alianguka dakika ya tatu (3) mjini Kota Bharu na kukimbizwa Hospitalini.
Mkurugenzi wa T-Team, Syahrizan Mohd Zain amesema Oniya alicheleweshwa kupata matibabu ya haraka.
"Alipata shinikizo la moyo uwanjani, ingekuwa stori nyingine kama dereva wa gari la kubebea wagonjwa angekuwepo  kwa haraka," Amewaambia New Straits Times.
"Dereva wa Ambulance alikuwa anaangalia mechi wakati Oniya anaanguka ghafla na beki wetu alikosa hewa kwa dakika nyingi".
Syahrizan amesema mechi ilivunjika dakika ya 60 baada ya kupokea taarifa za kifo cha Oniyo kutoka Hospitalini.
"Alitangazwa kufariki dunia hospitalini baada ya dakika 30" amewaambia Star newspaper.
Oniya amejiunga na klabu hiyo ya Malaysia msimu huu baada ya kucheza katika nchi za  Uzbekistan na Azerbaijan.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video