Ligi daraja la pili ya Argentina imeweka 'Headline' ya maana baada ya Alejandro Roncaglia, kaka wa mlinzi wa Fiorentina, Facundo Roncaglia, kumtandika ngumi kali mwamuzi Arnaldo Beron kufuatia kumuonesha kadi ya njano.

Roncaglia alichukizwa mno baada ya kuoneshwa kwadi na refa r Beron katika mechi ya Ferro na Tiro Federal.

Beron alipigwa na Roncaglia, ambaye baadaye alizuiliwa na wachezaji wanzake kuendeleza kichapo akipinga maamuzi ya reafa huyo.
Wachezaji walimkimbilia Beron aliyekuwa amepoteza fahamu na mara moja wakawaita watu wa huduma ya kwanza .
Mechi ilivunjika baada ya refa kupelekwa Hospitalini na gari la wagonjwa 'Ambulance'.
0 comments:
Post a Comment