Rais wa Espanyol, Joan Collet amefichua kwamba klabu yake na Real Madrid zimefikia makubaliano yatayomfanya Lucas Vazquez arejee tena Santiago Bernabeu.
Winga huyo amekulia katika mfumo wa soka la vijana la Real Madrid ambapo alijiunga akiwa na umri wa miaka 16, lakini alipelekwa Espanyol msimu uliopita.
Nyota huyo alifunga magoli matatu na kutengeneza sita katika mechi 33 za La Liga na Espanyol ilitaka kununua mkataba wake, lakini Madrid wameamua kumrejesha tena.
Timu hizo mbili zimekubaliana ofa inayoaminika kuwa Euro milioni moja sawa na paundi laki saba na elfu kumi.
0 comments:
Post a Comment