HATIMAYE Ramadhan Singano ‘Messi’ ameibwaga klabu yake ya
Simba na kutangazwa kuwa mchezaji huru katika kikao kilichofanyika leo makao
makuu ya shirikisho la Soka Tanzania, TFF, maeneo ya Karume, Ilala, Dar es
salaam.
Katika kikao hicho, Simba iliwakilishwa na mjumbe wa kamati
ya Utendaji na mwenyekiti wa kamati ya ufundi, Collins Frisch, wakati upande wa
Singano alikuwepo Singano mwenyewe na mwenyekiti wa Chama cha wachezaji
Tanzania, SPUTANZA, Musa Kisoky
huku TFF ikiwakilishwa na katibu mkuu
wake, Selestine Mwesigwa na msimamizi wa sheria na wanachama wa TFF, Eliud
Mvela.
Baada ya majadiliano ya pande zote mbili, huku kila mtu
akitoa vielelezo vyake, kikao hicho kimeamua kwamba mikataba yote miwili
imefutwa baada ya kuipitia, hivyo Singano na Simba waanze mazungumzo mapya.
KWANINI MIKATABA YOTE IMEFUTWA, UPI NI SAHIHI?
Hoja ya Msingi ni nani alichakachua
Mkataba?
Imebainika kuwa mkataba wa Singano aliosaini Mei 1, 2013 na
unaotakiwa kumalizika Julai 1, 2015 ndio sahihi, wakati ule wa Simba unaoonesha
ulisainiwa Mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika Julai 1, 2016 sio sahihi.
Kwa tafsiri rahisi, Simba ndio waliochakachua mkataba,
lakini kutokana na busara za TFF ambazo tunazishuhudia mara nyingi wameamua
kuwalinda Wakongwe hao wa soka la Tanzania.
Kwanini wasema mikataba yote haipo wakati kwenye mfumo wa
TFF mikataba yote ya wachezaji ipo?
Simba wamelindwa na TFF, lakini ukweli unabaki pale pale
kwamba mkataba wa Singano ndio sahihi, hivyo kisheria ni mchezaji huru baada ya
kushinda vita iliyogubikwa na kejeli na vitisho kutoka upande wa pili.
AKISHINDWA KUMALIZANA NA SIMBA KATIKA MAZUNGUMZO MPYA ITAKUWAJE?
Kama TFF wamewataka Singano na Simba kuzungumza upya kwasababu
mikataba yote imefutwa, maana yake wakishindwana, Singano anachukua hamsini
zake na sio lazima akubali kuendelea kuichezea Simba.
Wakati huo huo, mtandao huu umefahamishwa kuwa, Katibu mkuu
wa TFF, Mwesigwa amemuandikia barua Singano ambayo nakala yake amechukua
mwenyekiti wa SPUTANZA, Bwana Kisoky ikithibitisha
maamuzi yaliyochukuliwa na kuwa ushidi
wa maazimio ya kikao hicho.
Ukweli ni kwamba TFF wamemaliza kiaina ili wasiwaumbue Simba
waliokosea mkataba wao na wamewataka kufanya mazungumzo upya wakati ilitakiwa
watangazwe kuchakachua mkataba.
Simba wanajua fika kwamba mkataba wa miaka miwili wa Singano
ndio sahihi ndio maana wamekubali yaishe.
Endelea kufuatilia mtandao huu….tutakuletea Sinema nzima ya
suala hili…
0 comments:
Post a Comment