Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez amesafiri kwenda Cardiff kukutana na Gareth Bale kabla ya mshambuliaji huyo ghali zaidi duniani kuiongoza Wale kushinda bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji.
Mechi hiyo ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya (Euro 2016) ilipigwa jana na Bale ndiye aliyefunga goli pekee dakika ya 25.

Ripoti kutoka Hispania zinaeleza kwamba Benitez amepewa kazi maalamu ya kumrudisha Bale kwenye kiwango ili kuijenga upya Real Madrid kwasababu Cristiano Ronaldo mweye miaka 30 anakaribia kuanza kushuka.
Baada ya kutangazwa na utawala kuwa kocha mkuu wa Bernabeu, Benitez hajapoteza muda kuanza kazi na jana alipigwa picha katika Hoteli aliyopo Bale akimsalimia kabla ya kuzungumza naye baadaye.
0 comments:
Post a Comment