Jackson Martinez amechagua kutua kwa Miamba ya kandanda ya Seria A iliyosinzia kwasasa, AC Milan na atasaini kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 35.
Rais wa FC Porto, Pinto da Costa amethitibisha kuwa mchezaji huyo amempa taarifa hiyo kabla ya kwenda likizo.
Kwa maana hiyo, Arsenal watamkosa mchezaji huyo wanayemuwani majira haya ya kiangazi ingawa bado hawajatuma ofa kwa Mcolombia huyo ambae ameifungia Porto magoli 67 katika mechi 90 za ligi kuu.
Kutokana na Olivier Giroud kukosa cheche za maana katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal, Mfaransa, Arsene Wenger anaamini Martinez anaweza kuwa mshambuliaji wa maana na atampeleka Giroud kwa mkopo klabu nyingine.
Sasa itabidi Wenger aelekeze rada sehemu nyingine kwasababu Milani wapo tayari kutoa euro milioni 35 na tayari mchezaji ameonesha nia ya kutua klabuni hapo.
Tazama video inayoonesha magoli na ufundi wa Martinez akiwa na FC Porto
0 comments:
Post a Comment